Utamaduni


UTAMADUNI NI NINI?

Utamaduni ni jumla ya mambo yote yanayohusishwa na jamii. Ili kukidhi utashi wa maendeleo yake au utamaduni ni mwenendo wa maisha ya jamii, mtazamo wao wa mambo na taratibu zao za kuendesha maisha zinazowatofautisha wao na jamii nyingine.

 


UTAMADUNI WA WASIOSIKIA (VIZIWI)

Sisi  Viziwi tunao utamaduni wa pekee ya mawasiliano kwetu. Tunafanya mambo ambayo yanatofautiana na wanaosikia. Mfano wa utamaduni ulivyo:-


LUGHA

Lugha ya alama ni lugha ya dhamani sana kwetu katika mawasiliano. Ni lugha bora uliyobuniwa urahisi. Lugha hii huweza kutumika shuleni, hospitali, mikutanoni, n.k

Tunapokutana tunajadiliana kwa hii, tunajadili mambo mbalimbali, maisha, matangazo, siasa, amani  n.k.

Na lugha zilizopo nchini yaani lugha ya maandishi na matamshi  ni lugha za pili kwa mawasiliano kwetu. Tunajaribu kuzitumia kwa tabu ili kujenga mawasiliano, lakini kihistoria shule nyingi za viziwi hawajui njia za kufundishia kwa lugha ya alama. Lugha yetu ya alama inadhamani kubwa na ubora zaidi kwa kufundhisha kuliko lugha za nchini.


KUTUMIA MATAMSHI.

Mawasiliano kwetu na wanaosikia kimatamshi unatakiwa uzungumze polepole na matamshi yanayoeleweka bila kupaza sauti wala kusema kwa nguvu. Hatusikii bali tunaweza kusoma matamshi kwa macho, msemaji atatakiwa awe ana kwa ana na asiyesikia. Pawe penye mwanga wa kutosha. lakini hii itakuwa ngumu, uelewa wake ni asilimia chache sana tofauti na mawasiriano ya kutumia lugha ya Alama.


VITENDO

Vitendo au mwenendo wa Viziwi hutofautiana sana na wanaosikia, sio kimakosa bali ndivyo ulivyo katika mwenendo wa utamaduni wake (njia yake). Mfano wa vitendo kama wakati wa kutembea, kula, kuashiria na kuona. Wakati wa kutembea huburuza viatu na husababisha kutoa sauti, hii ni kutokana na kutokusikia na kurekebisha miguu iendavyo, wengine hutembea kwa kuyumba kama mlevi wakati wa usiku.

Wakati wa kula anaweza (tunaweza) kutafuna chakula kwa kutoa sauti, wakati wa kumengenya chakula tofauti na wanaosikia hutafuna akitoa sauti anarekebisha, upande wetu hatujui sauti itokavyo.

Wakati wa kuhashiria kuwasiliania wengine utoa ishara ambayo mtu akiona atafikilia amekasirika au mgomvi ila si hivyo ni desturi kawaida ya mawasiliano yetu. wakati wa kutembea barabarani au tukiwa mikutanoni bila mkalimani tunaangalia kila pande tukifikilia kuna kitu au magari nyuma. Wanaosikia wao hutembea bila kugeuza geuza kicha husikia na kujua kinachoendelea.


IBADA

 utamaduni katika ibada (kusali). Jamii yetu wasiosikia hutumia lugha ya alama ambayo ndio mawasiliano kwetu wakati Mchungaji au Mwinjilisti atasimama kuhubiri mbele ya madhabahu ili alama ionekane bila kikwazo kwani kusimama nyuma ya madhabahu huziba mawasiliano. Wakati wa kuomba Hatufumbi Macho kama Wanaosikia Bali tunanaangalia Alama kwani macho ndio yanakuwa masikio yetu.

 Mpangilio wa viti unaweza kuwa wa mduara kurahisisha mawasiliano Endapo tutakuwa wengi itabidi tukae kwa mpangiliomaalum yaani wafupi wanakuwa mbele ili tunaposimama inakuwa rahisi sana kuona alama.

 

 

Ukurasa Mkuu

Share